TIMU ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya miaka 17
‘Serengeti Boys’ jana imelazimishwa sare ya tasa dhidi ya Mali ikiwa ni mchezo
wa kwanza kwa AFCON U17 .
![]() |
Katika mchezo huo ulikuwa na ushindani kwa pande zote mabingwa
watetezi, Mali walimiliki mpira kwa muda mrefu jana, lakini wakashindwa
kuifunga Tanzania inayocheza mashindano ya ngazi hii kwa mara ya kwanza na
mwishowe wakatoka sare ya 0-0.
Matokeo mengine ya kundi B Angola ikalazimishwa sare yakufungana magol 2-2
na Niger .
Mechi za Kundi B zitarudi Alhamisi ya Mei 18,
Tanzania wakianza na Angola kabla ya Mali kupepetana na Niger Uwanja wa
l’Amitie Sino mjini Libreville.
Hatua ya makundi inatarajiwa kuhitimishwa Mei 20 na 21 mwaka huu, Kundi A
Gabon wakimaliza na Cameroon na Guinea na Ghana Uwanja wa Port Gentil kabla ya
siku inayofuata, Mali kuanza na Angola na baadaye Tanzania kumalizana na Niger.
Timu mbili za juu katika kila kundi pamoja na kwenda Nusu Fainali, pia
zitajihakikishia tiketi ya kucheza Fainali za kombe la Dunia la U-17 Oktoba
mwaka huu nchini India
No comments:
Post a Comment