Friday, 9 June 2017

JAMHURI YAJINATA KUTWAA UBINGWA LIGI KUU ZANZIBAR.



Timu kongwe katika historia ya soka la Zanzibar na vinara wa ligi kuu soka ya Zanzibar iliyopo katika hatua ya nane bora timu ya Jamhuri wamepania kuhakikisha watwaa ufalme wa soka nakuiwakilisha nchi kimataifa.

 
Kikosi cha vinara wa ligi kuu soka ya Zanzibar ,timu ya Jamhuri kutoka kisiwani Pemba.
Jamhuri ambao wamefanikiwa kujinyakulia alama tisa katika  michezo mitatu iliyocheza kabla yakuingia mapumzikoni kupisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani inaendelea na maandalizi kwa ajili ya ligi hiyo inayotarajiwa kuendelea tena July 9 ,mwaka huu.

Kocha wa vinara wa ligi kuu soka ya Zanzibar  Abdulmutik Haji 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kocha mkuu wa timu hiyo Abdumutik Haji imesema wanajipanga kuona wanamaliza ligi hiyo wakiwa vinara nakujinyakulia tiketi yakuiwakilisha nchi kimataifa.

“Unajua mimi naijua vizuri ligi ya Zanzibar pia vijana wangu wapo vizuri tunajianda kupambana ili kutwaa taji la ubingwa wa Zanzibar ,jambo ambalo linawezekana sana tu,tumeanza vizuri michezo hii ya hatua ya nane bora najua vijana wangu hawataniangusha ”alisema.

Ameongeza kuwa kasi ambayo kikosi chake hicho imeianza nayo katika ligi hiyo itaendelea nayo na imani yake kubwa nikufanya vyema kutokana na nyota ambao wapo katika kikosi chake wana ari yakujituma kufanya vyema katika michezo hiyo ya ligi kuu iliyosalia.

Akizungumzia soka la kisiwa cha Unguja na Pemba kocha huyo amesema hakuna tofauti kubwa timu za pande zote mbili zinalingana kinachopelekea timu za Pemba kuharibu katika misimu iliyopita ni maandalizi duni jambo ambalo katika kikosi chake kwa msimu huu halipo.

Jamhuri itaendelea kutafuta heshima yake July ,10 ambapo itakuwa mgeni wa timu ya Zimamoto mtanange ambao utavurumishwa katika uwanja wa Amani mnamo majira ya saa kumi alasiri.
                                                                    

No comments:

Post a Comment