Thursday, 1 June 2017

TUTARUDI NA UBINGWA ROLLING STONE,ASEMA NYOTA WA MIEMBENI CITY.

Mshambuliji wa Miembeni City aliyepo katika kikosi cha Combine ya wilaya ya mjini Ibrahim Abdallah(Imu Mkoko) amesema anamatumaini makubwa ya kikosi hicho kutwaa tena taji hilo.
Mshambuliji wa timu ya Miembeni City Ibrahim Abdallah akiwa katika mazoezi ya combine ya Rolling Stone.


Mkoko ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na mwandsihi wa habari hizi nakusema kuwa kutokana na uwezo wa wachezaji waliopo katika kikosi hicho sambamba na ari iliyopo anaimani wataibuka kidedea katika michezo hiyo.

“Nimeona wachezaji wote waliopo katika kikosi kile wanauwezo wa hali ya juu hivyo imani yangu tutaenda kupambana na kutetea taji ambalo tulitwaa katika mashindano yaliyopita kikubwa tunawaomba Wazanzibar watuombe ilitukafanye kile ambacho wanakihitaji “alisema mshambuliji huyo.

Akizungumzia ujio wa kiungo wa Kilimani City Asaad Juma Deco ambae walikuwepo pamoja katika kikosi cha Serengeti Boys ,Mkoko amesema kuwa ujio wa nyota huyo unazidi kuamsha ari katika kikosi hicho huku akisema kuwa mwalimu ameongeza mtu sahihi kwani kutokana na uzoefu alonao utasaidia kuimarisha uimara katika kikosi hicho.
MKOKO AKIWAJIBA KATIKA KIKOSI CHA SERENGETI BOYS.


Mkoko ambae amejiunga na kikosi hicho wiki hii akitokea Gabon katika mashindano ya mataifa ya Afrika kwa timu za vijana akiwa na Serengeti boys ameongeza kuwa juhudi na ari iliyopo kwa nyota wenzake sambamba na utayari wa viongozi bila shaka utaisaidia timu hiyo kuibuka ushindi katika michezo hiyo.


Mashindano ya Rolling Stone  inaendelea na mazoezi yake kujiandaa na mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kuanzia June 29 Jiji Arusha.

No comments:

Post a Comment