Aliyekuwa nahodha
wa timu ya taifa ya Zanzibar katika miaka ya 90 Shekha Khamis ameelezea
kufurahishwa na uwezo alionao mshambuliaji wa timu ya Zimamoto inayoshiriki
ligi kuu soka ya Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika alievaa jezi manjano akijaribu kumtoka Feisal Salum wa JKU. |
Kocha Shekha
ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema aina ya
uchezaji alionao Hilika unaenda na washambuliaji waliokuwepo katika kipindi
ambacho yeye akicheza soka.
Amesema anapomuona
nyota huyo akiwa uwanjani anamfananisha na Said Mwamba Kizota ambae alikuwa
mshambualiji hatari sana katika kipindi ambacho yeye akicheza soka.
Ameongeza kuwa
endapo nyota huyo ataendeleza kiwango chake alichonacho kutasamsaidia kufika
mbali zaidi kisoka.
Kocha Shekha
alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Zanzibar iliyotwaa ubingwa katika
mashindano ya Challenge mwaka 1995.
No comments:
Post a Comment