Thursday, 3 August 2017

Msimu wa 2017-2018 ;igi kuu soka ya Zanzibar kuanza October 1,Miembeni City,Charawe kushiriki kwa mara ya kwanza.

Chama cha mpira wa miguu visiwani kimekutana na vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja kupanga mikakati kadhaa  yakufanikisha msimu ujao wa ligi.

Katika kikao hicho kilichofanyika asubuhi ya leo katika kiwanja cha Amani pamoja na mambo mengine vilabu pamoja na ZFA wamekubaliana kuanza kwa msimu ujao October mwaka huu.

Sambamba na hayo vilabu vimetakiwa kuendelea na zoezi la usajili na uhamisho huku wakisisitizwa kulipia ada ya mashindano,ada ya mwaka kwa mrajisi wa vyama vya michezo sambamba na ada ya mwaka katika wilaya ambapo kila inatoka.

Akizungumza na viongozi wa vilabu 14 vinavyoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja rais wa chama cha mpira wa miguu visiwani Ravia Idarous amesema katika msimu ujao wa ligi hawataziruhusu kushiriki katika mashindano timu ambazo hazijalipia ada ya mashindano sambamba na ada zote ambazo vilabu vinatakiwa kulipa.

Ameongeza kuwa malipo yote hayo yanatakiwa kufanywa kupitia akauti ya ZFA iliyopo bank ya watu wa Zanzibar na baada yakulipia ada hizo wanatakiwa kufikisha ofisini risiti huku akisisitiza kuwa hakuna pesa itakayopokelewa mkononi.

Amewataka viongozi wa vilabu kufanya usajili katika kipindi kilichowekwa na chama chao hakitaongeza siku za usajili.

Kuhusu mfumo ambao utatumika kwa ajili ya msimu ujao wa ligi amesema utaendelea mfumo ule ule wa mwaka jana huku vilabu vikitakiwa kudumisha nidhamu katika michezo hiyo.

Vilabu 14 ambavyo vitashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja ni Chuoni,Blacksaloir,KVZ,KMKM,Mafunzo,Zimamoto,JKU,Kilimani City,Jang’ombe Boys,Taifa ya Jang’ombe,Kipanga, Charawe na Miembeni City.

No comments:

Post a Comment