Tuesday, 19 September 2017

KIPIGO CHAIPELEKA MIEMBENI CITY MAFICHONI.

Baada ya kipigo cha magol 2-0 kutoka kwa mabingwa wa ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya Miembeni City inatarajiwa kuingia kambini jioni ya leo September 20 kujiandaa na ligi kuu soka ya Zanzibar  kituo cha  Unguja inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake October 3 mwaka huu.
KIKOSI CHA MIEMBENI CITY KILICHOANZA KATIKA MCHEZO WA NGAO YA HISANI DHIDI YA JKU

Miembeni City ambao walipokea kipigo hicho katika mchezo wa Ngao ya Hisani uliovurumishwa jioni ya jana katika dimba la Amani mjini Unguja wameaamua kukaa kambi ilikupata muda wakutosha wakukiandaa kikosi hicho kuelekea msimu mpya wa ligi.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya timu hiyo vijana hao wanatarajiwa kuingia kambini jioni ya leo na hawatatoka hadi siku ya mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Polis mchezo ambao unatarajiwa kusukumwa katika kiwanja cha Amani mjini Unguja October 5 mnamo majira ya saa kumi alasiri.

No comments:

Post a Comment