Wednesday, 7 June 2017

Dulla boys kuipa mazoezi combine ya rolling stone.


Timu ya Dulla Boys  ya Jambiani wilaya ya kusini Unguja kesho inatarajiwa kupiga mchezo wa kirafiki na timu ya Combine ya wilaya ya mjini mtanange ambao utavurumishwa katika kiwanja cha Amani mjini Unguja mnamo majira ya saa mbili na nusu usiku.

Kocha mkuu wa combine ya wilaya ya mjini Muhamed Seif King.


Mchezo huo wa kirafiki ni maalum kwa combine ya wilaya ya mjini kujipima nguvu kuelekea mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kufanyika Mbulu Manyara kuanzia  July 7 mwaka huu.

Akizungumza na mtandao huo kocha mkuu wa timu ya combine ya wilaya ya mjini Muhamed Seif King amesema katika mchezo huo wa kirafiki anatarajiwa kumtumia mshambuliaji wake hatari Ibrahim Abdallah Mkoko ambae alijiunga na timu hiyo akitokea Gabon katika mashindano ya AFCON.

Ukiachia Mkoko kocha huyo amesema kuwa anatarajiwa pia kumtumia mshambuliaji wa timu ya Villa United Juma Ali Yussuf(James).
Wachezaji wa combine ya wilaya ya mjini baada ya mazoezi 


Ameongea kuwa kikosi hicho kitaendelea kucheza michezo ya kirafiki kila mwezi mara mbili ilikukieka sawa kikosi chao hicho.


Aidha kocha King amewataka washabiki na wapenzi wa soka visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ilikuona viwango vya vijana wake ambao wamepania kufanya vyema katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment