Wednesday, 7 June 2017

Assad Juma(DECO) aomba kuondolewa combine ya rolling stone.


Kiungo wa timu ya Kilimani City Asaad Juma (DECO) ameomba kuondolewa katika kikosi cha Rolling Stone kinachotarajiwa kushiriki katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Mbulu Manyara kuanzia  July 7 mwaka huu.
Kiungo Assad Juma akiwa katika majukumu ya taifa na Serengeti Boys.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kocha mkuu wa timu hiyo Muhamed Seif King imesema sababu kuu iliyopelekea kuomba kujindoa katika kikosi hicho nikutokana na nyota huyo kuhitaji kupumzika kutokana nakufanya kazi sana katika timu ya taifa ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys.

“Unajua Ibny Asaad tulimuita akatukubalia kujiunga na kikosi lakini baada ya mazoezi ya siku mbili akaomba kupumzika na uongozi umemkubalia nakumpa baraka zote tunamshukuru ametuheshimu tulipomita katika kikosi chetu”alisema King.
Kiungo wa timu ya Kilimani City Asaad Juma akiwa na jezi ya Serengeti Boys.


Ameongeza kuwa kumruhusu kuondoka katika kikosi hicho kwa kiungo huyo hakutoathiri chochote katika kikosi chao hicho na anamatumaini makubwa yakuona kikosi chao kinafanya vyema katika mashindano hayo.


Kikosi cha Combine ya wilaya ya mjini kinatarajiwa kuondo visiwani Zanzibar kuelekea Mbulu Manyara ,Tanzania bara July 4 mwaka huu tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment