Tuesday, 18 July 2017

Taifa ya Jang’ombe,Jang’ombe Boys na JKU waifukuzia huduma ya Boban.

Ikiwa ni siku mbili tokea kufunguliwa kwa zoezi la usajili na uhamisho visiwani Zanzibar viongozi wa vilabu vitatu tofauti vimekuwa vikihaha kuihitaji huduma ya kiungo hatari wa Miembeni City Haroun Abdallah Jabir(Boban)
Haroun Abdallah akijifua katika fukwe za Kibiji kujiejka sawa na msimu ujao wa ligi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ambazo mtandao huu umezinasa tayari vilabu hivi vikubwa kwa sasa visiwani hapa wameshatuma watu wao kuanza kwa mazungumzo na nyota huyo ambae alikuwa msaada mkubwa katika timu yake hiyo.

Juhudi zakumpata kiungo huyo zimepatikana nakuthibitisha kutakiwa na vilabu hivyo vitatu nakusema yeye yupo tayari kucheza popote pale jambo la msingi ni maslahi yake sambamba nakufikia makubaliano na timu yake ya sasa ambayo anamkataba nayo wa miaka mitatu.

Aidha kiungo huyo hatari wa timu ya Miembeni City ameanza mazoezi madogomadogo yakujieka sawa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Boban ambae yupo mapumzikoni Tanzania bara ameanza mazoezi hayo mepesi yakujieka sawa tayari kwa msimu ujao wa ligi katika fukwe za Kibiji jijini Dar es salam.

Akizungumza na mtandao huo kiungo huyo ambae alikuwa chachu ya mafanikio katika timu yake hiyo amesema ameamua kuanza mazoezi ilikuuweka sawa mwili wake tayari kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Ameongeza kuwa anajipanga kuona anaisadia timu yake kufanya vyema katika msimu mpya wa ligi nakufanya vyema zaidi kama walivyofanya msimu uliopita.



No comments:

Post a Comment