Kocha mkuu
wa timu ya chuo cha waandishi wa habari Zanzibar Abubakary Hatibu Kisandu
amesema vijana wake wapo vizuri kwa ajili ya mashindano ya vyuo vikuu na
taasisi ya elimu ya juu Zanzibar yanayotarajiwa kuanza Jumapili May 14 mwaka
huu.
Akizungumza na
zenjsport on –line kocha huyo amesema vijana wake wapo vizuri na wanaendelea na
mazoezi huku kikosi chake cha mwaka huu kimesheheni nyota kadhaa ambao
wanauwezo wa hali ya juu katika kusakata soka.
Akiwataja baadhi
ya nyota ambao wapo katika kikosi chake ni pamoja na kiungo anaekipiga timu ya
Taifa ya Jang’ombe Muhamed Said ‘Messi’,mshambuliaji wa timu ya Polisi Khamis Maulid
na nyota kadhaa ambao wanatarajiwa kuonesha kandanda safi katika mashindano
hayo.
![]() |
Kocha wa timu ya Chuo cha uandishi wa habari Abubakary Hatibu alievaa shuti nyeusi akiwa katika picha ya pamoja na nyota wa timu hiyo. |
Ameongeza kuwa
lengo lake kama mwalimu nikuona timu inachukua ubingwa katika mashindano hayo
ambayo katika msimu uliuopita walitolewa katika hatua ya makundi.
Sambamba na
hayo Kisandu amesema kuwa uongozi wa chuo umeongeza posho kwa wachezaji ili
kumasha ari zaidi nakuifanya timu ifanye vizuri katika mashindano hayo ya
Zahilfe Cup.
Katika mashindano
yaliyofanyika mwaka jana Chuo cha Uandishi wa habari Zanzibar kilitolewa katika
hatua ya makundi baada yakupokea kipigo katika michezo yote ya hatua hiyo
ambapo walifungwa na magol 4-0 na Sumait,3-0 na Microtech nakumaliza ka kipigo
cha magol 2-1 kutoka kwa timu ya ICPS.
No comments:
Post a Comment