TIMU ya Jeshi la Kujenga
Uchumi (JKU) ya Zanzibar itaanza na Zesco United ya Zambia katika Raundi ya
Awali ya ligi ya mabingwa Afrika.
JKU SC wataanzia nyumbani
Uwanja wa Amaan, Zanzibar kabla ya kusafiri hadi Ndola kwa mchezo wa marudiano.
Katika droo iliyofanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu 59 zimepangwa katika Ligi ya Mabingwa na 54 zimo katika Kombe la Shirikisho.
Mashirikisho ya nchi nane tu hayajawasilisha wawakilishi ambayo ni ya Cape Verde, Chad, Eritrea, Namibia, Reunion, Sao Tome and Principe, Sierra Leone na Somalia.
Mbona huna taarifa siku hizi
ReplyDelete