Saturday, 11 November 2017

WAZIRI RASHID AWATAKA NYOTA ZANZIBAR HEROES KUJITUMA KWA MOYO WAO WOTE.

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Rashid Ali Juma amewataka wachezaji waliopo katika timu ya taifa ya Zanzibar ( Zanzibar Heroes) kujituma kwa moyo wao wote ilikuviletea heshima visiwa vya Zanzibar.

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo Rashid Ali akizungumza na wachezaji wa Zanzibar Heroes hawapo pichani.


Waziri Rashid ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wachezaji wa timu hiyo wakati alipotembelea katika mazoezi ya timu hiyo.

Amesema endapo vijana hao watajituma kwa moyo mmoja kuanzia sasa timu ikiwa katika maandalizi na wakati wa mashindano timu hiyo itatwaa ubingwa wa mashindano hayo.
Baadhi ya wachezaji wakimsikiliza waziri wa habari.

Ameongeza kuwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo na baraza la michezo watatoa ushirikiano wao wa hali na mali ilikuifanya timu hiyo kuwa na maandalizi yakutosha.

Nae katibu wa chama cha mpira wa miguu visiwani hapa Muhamed Ali Hilal Tedy amesema chama chao kimejipanga kuona wanaindaa timu hiyo katika mazingira yaliyo bora.

Amesema changamoto kuu ambayo kwa sasa wanakabiliana nayo nikukosekana kwa baadhi ya wachezaji ambao wanacheza ligi kuu Tanzania bara sambamba na ukata wa fedha.
Waziri wa habari akiwa na mwenyekiti wa baraza la michezo ,rais wa ZFA ,katibu mkuu wa ZFA na mkurugenzi wa ufunzi wa ZFA wakifuatilia mazozei ya timu ya taifa ya Zanzibar asubuhi ya leo.

Aidha amewataka wadau wa soka kuunga mkono juhudi za chama chao ilikufanya maandalizi yakutosha kwa timu hiyo
Timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) inajiandaa na mashindano ya Afrika mashariki na kati yanayotarajiwa kufanyika nchi Kenya mwishoni mwa mwezi huu nchini Kenya..

No comments:

Post a Comment