Kufuatia kucheza
michezo mitano nakupoteza katika michezo yote uongozi wa timu ya Charawe imemteua kocha Ali
Bushir kukinoa kikosi chao hicho katika michezo iliyosalia.
Hayo yamethibitishwa
na katibu wa timu hiyo Haji Bakar wakati alipokuwa akizungumza nasi nakusema
wana imani kubwa kocha huyo anaisadia timu yake ifanye vyema.
Amesema kuwa
anamatumaini makubwa timu itafanya vyema kufuatia ujio wa kocha huyo ambae
amekuwa na uzoefu katika ligi kuu ya Zanzibar.
Ameongeza kuwa kocha
huyo amekubali kufanya kazi katika kikosi hicho nakuahidi kutoa mashirikiano ya
hali ya juu katika kikosi chao hicho.
Charawe ambayo inashiriki
kwa mara ya kwanza ligi kuu soka ya Zanzibar tayari imeshacheza michezo mitano
nakupoteza katika michezo yote mitano.
No comments:
Post a Comment