Kocha Mkuu wa timu ya
Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman (Morocco)
amemuongeza kwenye kikosi Mshambuliaji wa Lipuli ya Iringa Seif Rashid Abdallah
(Karihe) ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo itakayokwenda Kenya katika Mashindano
ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba
9, 2017.
Katika uteuzi wa awali
wa wachezaji 30 Karihe hakuitwa lakini kocha Morocco amelazimika kumuongeza
mshambuliaji huyo na atakuwa mchezaji wa 31 kuitwa katika kikosi cha awali huku
Morocco akisema si kosa kwa timu ya Taifa kupunguza au kuongeza mchezaji wakati
wowote tu ikiwa bado haijaenda katika Mashindano.
“Hii ni timu ya Taifa
wakati wowote unamwita mchezaji au unamtoa kutokana na mahitaji yako,
nimelazimika kumuongeza Karihe kwasasa ataungana na wenzake 30 wale wa awali”.
Alisema Morocco.
Wakati huo huo kikosi
cha timu ya taifa ya Zanzibar kimeendelea na mazoezi yake asubuhi ya leo
kuendelea namazoezi nyake kujiandaa na mashindano hayo chini ya mwalimu wake
Hemed Suleiman Morroco.
Wachezaji waliyoanza
mazoezi ni wale ambao vilabu vyao vya Unguja huku ikiwa bado makundi mawili
kutoka Kisiwani Pemba na Tanzania Bara bado hawajajumuika na wenzao ambapo wale
kutoka Pemba wakitarajiwa kesho kuungana na wenzao.
Wachezaji waliyoanza mazoezi ni Walinda mlango Ahmed Ali
"Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman
"Wawesha" (JKU), Walinzi Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm
Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz"
(Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya
Jang'ombe).
Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul
Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad
Mshamata (Chuoni) pamoja na washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe)
Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais"
(Jang'ombe boys) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).
No comments:
Post a Comment