Baadhi ya wadau wa soka visiwani
Zanzibar wameelezea kufurahishwa kwao na mwenendo nzuri wa timu ya soka ya
kanda ya Unguja iliyopo katika mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za
Sekondari Tanzania (UMISSETA) yanayoendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu
Butimba mkoani Mwanza.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wadau hao wamesema wanafurahishwa na kile kinachofanywa na wanandinga hao huku
wakijua wanashiriki mashindano hayo wakiwa katika wakati mgumu kutokana na
asilimia kubwa ya vijana hao wanashiriki katika michezo hiyo wakiwa na funga.
Mwalimu Othman Hamad Bakari mwalimu
wa michezo skuli ya Mtoni ameuambia mtandao huu kuwa yeye binafsi anafurahishwa
na matokeo mazuri ambayo vijana hao wanayapata nakuwaomba wadau wa soka
kuwaombea vijana hao ilikufanya vyema zaidi nakuja na kikombe cha michezo hiyo.
“Ni mwanzo nzuri ,timu imeshinda
katika michezo miwili tena kwa wastani nzuri tu wa magol yakufunga jambo la
muhimu kwetu nikuwaombea vijana wetu warudi na ushindi wanacheza katika
mazingira magumu sana, najua asilimia kubwa ya wanamichezo wetu wapo katika
mfungo “alisema mwalimu huyo.
Vijana wa kanda ya Unguja watajitupa
dimba leo hii Jumamos June,10 mnamo majira ya saa sita na nusu za mchana
kumenyana na Mara,ambapo vijana hao wanajitupa katika mchezo huo wakiwa na
rekodi nzuri ya ushindi katika michezo iliyopita ambapo waliifunga Katavi 4-0, Kagera
3-0 wanahitaji ushindi katika mchezo wa leo ilikusonga mbele katika hatua
nyengine.
Kikosi cha kanda ya Unguja kilichopo Mwanza katika mashindano ya UMISETA. |
Michezo mengine kwa upande wa timu
ya soka ya kanda ya Unguja ukiachia ule wa mchana wa leo dhidi ya Mara mnamo
majira ya saa 6:30 za mchana wa leo ni ule wa Jumapili June 11, 2017 dhidi ya
Mbeya, Jumatatu June 12, 2017 Unguja dhidi ya Iringa, Jumanne June 13, 2017
Unguja watamalizana na Dar es salam.
Huku kikosi cha kanda ya Unguja
kikiwakilishwa na walinda milango Aley
Ali Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu).
Huku kwa upande wa walinzi wakijumuishwa na Ibrahim
Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious), Abubakar Khamis
(Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba),
Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya.
Kwa upande wa viungo kikosi hicho
kinaundwa Amani
Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji Suleiman
(JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni) na
Eliyasa Suleiman (K-pura).
Huku safu ya washambuliaji
ikiwajumuisha Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan
(Bububu), Walid Abdi “Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali Omar
(Mwera).
No comments:
Post a Comment