Katika kuhakikisha
wanafanya vyema katika msimu ujao wa ligi timu ya Gulio FC inyoshiriki ligi
daraja la pili wilaya ya mjini Unguja inaendelea na mipango yake yakuimarisha kikosi chao hicho.
![]() |
Washabiki wa taifa ya Jang'ombe |
Akizungumza na
mtandao huu rais wa timu hiyo Ahmed Khamis amesema timu yao inaendelea na
mazungumzo na nyota kadhaa ambao wataongeza nguvu katika kikosi chao hicho.
Amesema kuwa
kutokana na mipango ya mwalimu timu hiyo inatarajiwa kuanza mazoezi rasmini
yakujiandaa na msimu ujao wa ligi Jumatatu June 12.
![]() |
Wachezaji wa Guluion wakishangiria katika moja ya michezo ya ligi daraja la pili wilaya ya mjini katika msimu uliopita. |
Aidha ameongeza
kuwa katika kuonesha wanawajali wapenzi wa timu hiyo timu yao itakipiga mchezo
wa kirafiki na timu ya taifa ya Jang’ombe mtanange ambao utapingwa siku ya Idd pili katika uwanja wa Amnai Mjini Unguja huku mipango kwa ajili ya
mchezo huo wa kirafiki yakiendelea vizuri.
Amefafanua kuwa
kutokana na report ya mwalimu tayari uongozi umejua matatizo yaliyopelekea
kutokufanya vyema katika timu yao na tayari uongozi wa timu wanayafanyia kazi
mapungufu hayo.
No comments:
Post a Comment