Wednesday, 31 May 2017

LUGHA ,KIWANGO CHA ELIMU UTATA RASIMU YA KATIBA ZFA.

Na:Abubakry Hatibu

Ikiwa ni siku chache zimepita tokea kamati iliyoundwa kutengeneza katiba ya chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kukabidhi rasimu hiyo kwa katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar baadhi ya viongozi wa ZFA wa mawilaya wameanza kuonesha hofu yao juu ya rasimu hiyo.


Wakizungumza na zenjsport-on line kwa nyakati tofauti baadhi ya Viongozi hao wamesema ni vigumu sana kupita rasimu hiyo kwani ina mapungufu mengi sana huku wakitaja la kiwango cha elimu nakuandikwa kwa lugha ya kigeni.

“Hii Rasimu ina vichekesho sana tulipoiona tulishtuka, sisi viongozi ati tuwe na elimu kuanzia Form IV, kisha imeandikwa kwa Kiengereza wakati sisi ni Waswahili!, si rahisi kupita mazali na sisi ni miongoni mwa wapitishaji, kwasababu uongozi si kusoma bali uongozi ni kipaji na mapenzi ya kitu”.

Akizungumzia hali hiyo katibu wa kamati iliyoteuliwa kuunda katiba hiyo ambae pia ni mwanasheria wa ZFA Saleh Ali Said
Amewatoa wadau hao wa soka kuisoma kwa makini rasimu hiyo sambamba nakutomapungufu yaliyomo katika rasimu hiyo ili ipatikane katiba iliyobora zaidi ambayo inaendana na CAF.


Kamati ya kuandika katiba mpya inaundwa na wajumbe sita (6) ambao ni Afan Othman Juma (Mwenyekiti), Saleh Ali Said (Katibu), Othman Ali Hamad (Msaidizi Katibu), Nassra Juma, Eliud Peter Mvella na Ame Abdallah  Dunia.

1 comment: