Na:Abubakry Hatibu
Ikiwa ni siku chache
zimepita tokea kamati iliyoundwa kutengeneza katiba ya chama cha mpira wa miguu
visiwani Zanzibar kukabidhi rasimu hiyo kwa katibu mkuu wa chama cha mpira wa
miguu visiwani Zanzibar baadhi ya viongozi wa ZFA wa mawilaya wameanza kuonesha
hofu yao juu ya rasimu hiyo.
Wakizungumza na
zenjsport-on line kwa nyakati tofauti baadhi ya Viongozi hao wamesema ni vigumu
sana kupita rasimu hiyo kwani ina mapungufu mengi sana huku wakitaja la kiwango
cha elimu nakuandikwa kwa lugha ya kigeni.
“Hii Rasimu ina
vichekesho sana tulipoiona tulishtuka, sisi viongozi ati tuwe na elimu kuanzia
Form IV, kisha imeandikwa kwa Kiengereza wakati sisi ni Waswahili!, si rahisi
kupita mazali na sisi ni miongoni mwa wapitishaji, kwasababu uongozi si kusoma
bali uongozi ni kipaji na mapenzi ya kitu”.
Akizungumzia hali hiyo
katibu wa kamati iliyoteuliwa kuunda katiba hiyo ambae pia ni mwanasheria wa
ZFA Saleh Ali Said
Amewatoa wadau hao wa
soka kuisoma kwa makini rasimu hiyo sambamba nakutomapungufu yaliyomo katika
rasimu hiyo ili ipatikane katiba iliyobora zaidi ambayo inaendana na CAF.
Kamati ya kuandika katiba mpya inaundwa na wajumbe sita (6)
ambao ni Afan Othman Juma (Mwenyekiti), Saleh Ali Said (Katibu), Othman Ali
Hamad (Msaidizi Katibu), Nassra Juma, Eliud Peter Mvella na Ame Abdallah
Dunia.
Mwanzo mzuri katiba Bora ni muhimu sio bora katiba
ReplyDelete