Tuesday, 19 September 2017

JKU wawakaribisha Miembeni City ukubwani,yatwaa Ngao ya hisani.

Mabingwa wa ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya JKU imefanikiwa kutwaa Ngao ya jamii baada yakuifunga timu ya Miembeni City magol 2-0 katika mtanange uliovurumishwa katika dimba la Amani mjini hapa jioni ya jana.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani na wakuvutia nakushihudiwa na mashabiki lukuki kiwanjani hapo JKU walijipatia magol yao kupitia kwa  Salum Mussa na Nassor Mattar.

Mchezo huo unaashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi ambapo ligi kuu soka ya Zanzibar ikitarajiwa kutimua vumbi lake kuanzia October 3,kwa michezo miwili JKU wakikipiga na Mafunzo huku Jang’ombe boys wakimenyana na KMKM.


No comments:

Post a Comment