Wednesday, 13 September 2017

MIEMBENI CITY USO KWA USO KWA JKU KATIKA MCHEZO WA NGAO YA JAMII.

Mabingwa wa ligi daraja la kwanza taifa Unguja kwa msimu wa 2016-2017 timu ya Miembeni City inatarajiwa kukipiga na mabingwa wa ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya JKU katika mchezo maalumu wa ufunguzi wa ligi hiyo.

Mchezo huo ambao utavurumishwa katika dimba la Amani mjini hapa September 19 mnamo majira ya saa kumi alasiri unatarajiwa kuwa na ushindani kwa pande zote.
Afisa habari wa timu ya Miembeni City Ali Khamis Ibny amesema vijana wao wanaendelea kujinoa kufanya vyema katika mchezo huo huku mwalimu akiendelea kukinoa kikosi hicho ilikufanya vyema katika mchezo huo sambamba na ligi kuu soka ya Zanzibar.
Amesema hamu na hamasa kwa wachezaji wao imeimarika huku wakionekena kujituma zaidi katika mazoezi ilikufanya vyema katika mchezo huo sambamba na ligi kuu soka ya Zanzibar ambayo timu itashiriki kwa mara ya kwanza.

Ameongeza kuwa mchezo huo wa Ngao ya jamii kati ya timu yao hiyo na JKU utasaidia kuangalia mapungufu yaliyopo katika kikosi chao hicho kabla yakuanza kwa ligi kuu soka ya Zanzibar ambayo inatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
Mchezo  huo kati ya mabingwa wa ligi darajala la kwanza taifa Unguja kwa msimu wa 2016-2017 timu ya Miembeni City na mabingwa wa ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu 2016-2017 timu ya  JKU unaashirikia kuanza kwa msimu mpya wa ligi wa 2017-2018.

No comments:

Post a Comment