Timu ya
Miembeni City imekamilisha usajili wa mlinda mlango nambari moja wa timu ya
Zantex ,Ally Rajab ambae amesaini kandarasi ya miaka miwili na timu hiyo.
![]() |
Ally Rajab akisaini kandarasi ya miaka miwili na Miembeni City huku akishuhudiwa na aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi wa timu Ali Muhamed. |
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa habari wa timu hiyo Ali Khamis imesema
usajili huo unaifanya timu hiyo iwe na walinda milango watatu ambao ni Aley Ali
Suleiman,Abaas Wadi Makame na Ali Rajab alikuja kuongeza nguvu katika eneo
hilo.
Ali Rajab
anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Miembeni City katika kipindi hichi cha
usajili ambapo wiki iliyopita walimsajili mshambuliji ya Faisal Riam Lucas (Nado)
ambae amesaini kandarasi ya miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment