Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo wa serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Rshid Ally Juma amewataka wachezaji wa combine ya wialaya
ya mjini kuongeza bidii ilikuimarisha vipaji walivyobarikiwa na muumba.
![]() |
Waziri wa habari utamaduni ,utalii na michezo Rashid Ally Juma akizungmza na wachezaji wa timu ya combine ya wilaya ya mjini. |
Waziri Rashid ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na
wachezaji na viongozi wa timu hiyo huko ofisini kwake waliponda kupeleka kombe
waliotwaa katika mashindano ya Rolling stone yaliyofanyika Mbuu Manyara .
![]() |
Wachezaji wa combine ya wilaya ya mjini na viongozi wao wakimsikiliza waziri. |
Aidha amewapongeza vijana hao kwa ujasiri wa waliouonesha katika mashindano hayo licha ya changamoto kadhaa walizokabiliana nazo wakiwa katika mashindano hayo.
Ameongeza kuwa vijana hao walionesha nidhamu
ya hali juu na ndo jambo pekee lililowasaidia kuweza kutwaa Ubingwa huo.
Mapema mwenyekiti wa chama cha
mpira wa miguu wialaya ya mjini Unguja Hassan Haji Hamza ameiomba serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar kutoa michango yao ya hali na mali pindi timu itakapokuwa
na amshindano nje ya Zanzibar ilikuondoa changamoto ambazo hujitokeza.
No comments:
Post a Comment