Saturday, 29 July 2017

Central mjini yamaliza kwa mafanikio.

Mashindano ya vijana ndani ya wilaya ya mjini yamefikia tamati jana ambapo mabingwa katika madaraja mbalimbali walikabidhiwa zawadi zao.

Akizungumza na mtandao huu mara baada yakumalizika kwa mashindano hayo mwenyekiti wa kamati ya amshindabo hayo Khamis Machano amesema mashindabo hayo yamekwenda vyema licha ya changamoto kadhaa mabazo zinawakabili katika kuendesha michezo hiyo.

Akielezea changamoto ambazo wanakabilina nazo katika uendeshaji wa michezo hiyo mwenyekiti huyo amesema uhaba wa fedha imekuwa changamoto kubwa ambayo wanakabiliana nayo katika kuendesha mashindano hayo sambamba na idadi ndogo ya wajumbe wanaosimamia mashindano hayo ukilinganisha na timu ambazo zinashiriki katika michezo hiyo.

Akizungumzia suala zima la zawadi mwenyekiti huyo amesema mashindano ya mwaka huu zawadi ya fedha imepungua ukilinganisha na mwaka jana kutokana na shughuli mbalimbali ambazo kamati yao iliziendesha katika kipindi cha msimu uliomalizika jana.

“Unajua zawadi ya fedha imepungua ukilinganisha na mwaka jana kutoka na shughuli mbali mbali ambazo kamati iliendesha ,msimu huu tuliendesha kozi ya ukocha na kamati ndio iliyogharamia kwa asilimia kubwa kozi hiyo pia kamati ilichangia kwa asilimia kubwa timu ya vijana iliyoenda Manyara katika mashindano ya Rolling stone jambo ambalo limepelekea kamati kupunguza zawadi ya fedha ukilinganisha na mwaka jana”alisema.

Akizungumza vitendo vya upangaji matokeo uliojitokeza katika mashindano ya mwaka huu mwenyekiti huyo ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo hivyo huku akiwaomba wanaosimamia timu za vijana kuachana na vitendo kama hivyo kwani kunarejsha nyuma maendeleo ya soka la vijana.

Mabingwa katika madaraja mbalimbali kwa wilaya ya mjini ni kama ifuatavyo ,Junvinile mabingwa Gold win huku makamo bingwa wakiwa Blacksaloir,Juniour bingwa Tothham makamo bingwa Simba FC,mashindano ya mtoanao Juvinile bingwa Blacksaloir huku makamo bingwa akiwa New academy.


Kwa upande wa mashindano ya mtoano central  bingwa ni Villa coast na kwa upande wa mashindano ya mtoano Juniour bingwa ni Al-noour.

No comments:

Post a Comment