Thursday, 6 July 2017

JKU,JANG’OMBE BOYS WAZIFATA ALAMA TATU PEMBA.

Timu ya Jang’ombe boys pamoja timu ya JKU wanaondoka kisiwani Unguja kuelekea Pemba asubuhi hii kwa ajili ya michezo yao miwili ya ligi kuu soka ya Zanzibar.
 
Kikosi cha timu ya Jang'ombe boys .
Nyota hao wanaondoka visiwani kwa Meli ya MV Mapinduzi huku hali za nyota wa timu hizo wakiwa katika hali nzuri.

Ali Othman Kibichwa Rais wa timu ya Jang;ombe boys amesema wanaenda kisiwani Pemba kupambana nakutafuta alama tatu katika kila mchezo huku akisisitiza kuwa hawatazarau mchezo hata mmoja.

Kwa upande wake katibu wa timu ya JKU Saad Ujudi amesema wanuzeofu mkubwa na michezo ya aenda kisiwani huko kufanya vyema huku wakihitaji kushinda katika kila mchezo ilikujieka katika nafasi mbili za juu nakuiwakilisha nchi kimataifa.
 
Wachezaji wa timu ya JKU.
Jang’ombe boys wanatarajiwa kujitupa katika kiwanja cha Gombani kisiwani Pemba,July 9 kumenyana na timu ya Mwenge kutoka Wete kaskazini  mwa kisiwa cha Pemba.

Huku timu ya JKU ikitarajiwa kujitupa katika dimba hilo hilo la Gombani kisiwani Pemba ,July 10 kumenyana na timu ya Okapi michezo yote miwili ikichezwa mnamo majira ya saa kumi alasiri.


No comments:

Post a Comment