Friday, 7 July 2017

Jang’ombe boys wapokelewa kishujaa Pemba,Jamhuri kama Man U Amani.



Timu ya Jang’ombe boys imewasili kisiwani Pemba mchana wa jana tayari kwa ajili ya michezo yake ya ligi kuu soka ya Zanzibar inayoendelea wiki hii. 

Baadhi ya washabiki waliojitokeza kuilaki timu ya Jang'ombe boys kisiwani Pemba.

Boys ambayo imewasili katika bandari ya mkoani mnamo majira ya saa saba mchana huku ikipokelewa na mashabiki lukuki bandaria hapo ambao walijitokeza kuilaki timu hiyo.

Akizungumza nasi baada yakuwasili bandarini hapo rais wa mashabiki wa timu ya Jang’ombe boys kisiwani Pemba Hussein Shaaban amesema amefurahishwa na ujio wa timu yao hiyo nawatahakikisha wanaisapoti  ilikufanya vyema katika michezo yake ya ligi kuu soka itakayochezwa kisiwani hapo.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Jang'ombe boys wakiwasili katika bandari ya mkoani kisiwani Pemba.

Ameongeza kuwa ujio wa timu yao hiyo ni faraja kubwa kwao huku akiwapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kujituma kwao nakuhakikisha timu inafanikiwa kutinga hatua ya nane bora nakuwapa nafasi washabiki wa timu waliopo kisiwani Pemba kuishuhudia ikiwa uwanjani katika michezo ya ligi.

Nayo timu ya Jamhuri kutoka kisiwani Pemba inaendelea na maandalizi yake kujiandaa na mchezo wao wa ligi kuu soka ya Zanzibar dhidi ya timu ya Zimamoto mtanange ambao utavurumishwa katika dimba la Amani mjini Uguja.

Huku timu hiyo ikiendelea na maandalizi hayo kitu chakufurahisha ni mashabiki wanajitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu hiyo.

Kocha wa timu hiyo Abdulmutik amesema vijana wake wanaendelea na mazoezi kujiandaa na michezo ya ligi kuu huku akifurahishwa na hamasa waliyonayo washabiki wanaojitokeza uwanja kuwaunga mkono katika mazoezi yao.

 








No comments:

Post a Comment