Mabingwa watetezi wa
Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone timu ya Kombain
ya Mjini Unguja wameanza vyema kampeni za kulitetea taji walilotwaa mwaka jana
baada ya kuwafumua wenyeji wao timu ya Mbulu All Stars mabao 4-0 mchezo
uliopigwa katika uwanja wa Julius Nyerere huko Mbulu Mkoani Manyara.
Katika mchezo huo
ambao ulikuwa na ushindani kwa pande zote magoli ya washindi yalifungwa na Mohd
Vuai “Prince”, Seif Said “Tiote”, Abdul hamid Juma (Samatta) na Fahmi Salum
(Migwel).
Kikosi kilichoanza cha
combine ya wilaya ya mjini katika mchezo wa jana ni George Munish,Hassan
Chalii,Muharami Khamis,Abubakary Ame,Ali Juma,Muhamed Yahya ,Abrahaman
Juma,Yakoub Amour,Muhamed Vuai,Ibrahim Abdallah,Seif Said.
Sub .
Ali Mbarouk,Muhamed
Jailan,Mohamed Haji,Suleiman Ali,Fahmi Salum,Abdulhamid Juma na Muhamed Chafu
Mjini watashuka tena
Dimbani siku ya Jumanne ya July 11, 2017 kucheza na Kenya saa 8:00 za
mchanakatika uwanja wa Julius Nyerere huko Mbulu Mkoani Manyara.
No comments:
Post a Comment