Timu ya Charawe
imeianza vibaya ligi kuu soka ya Zanzibar kituo cha Unguja baada yakupokea
kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa timu ya KVZ mchezo ambao umevurumishwa mnamo
majira ya saa kumi alasiri katika kiwanja cha Amani mjini Unguja.
Goli lililopeka kilio
kwa Charawe limefungwa na
Rafael Mwambeleko
mnamo dakika ya 65 ya mchezo huo.
Na katika mchezo
uliochezwa mapema mnamo majira ya saa nane mchana timu ya Kilimani City ikaibuka
na ushindi wa magol 3-1 dhidi ya timu ya Kipanga.
Mabao ya City
yamefungwa na Bakar Bakar Mashango dakika ya 26, Joseph Josephat Kalinga dakika
ya 49 na Abdillah Seif Bausi dakika ya 85.
Bao pekee la Kipanga
limewekwa nyavuni na Nassor Ali katika dakika ya 90 ya mchezo.
Ligi kuu soka ya
Zanzibar kanda ya Unguja itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili
katika uwanja wa Amaan.
Saa 10 za jioni wataanza kati ya Maafande wa
Polisi kwa kucheza na Miembeni City, na saa 1 za usiku watakipiga Taifa ya Jang’ombe
dhidi ya Zimamoto.
No comments:
Post a Comment