Katika kuhakikisha
kinaendesha mashindano yake kwa uweledi na ufanisi wa hali ya juu chama cha
mchezo wa wavu Zanzibar kimeandaa mafunzo kwa waamuzi wanaocheza michezo hiyo
ilikutekeleza majukumu yao kwa uweledi.
Akizungumzia mafunzo
hayo katibu wa chama hicho Mwalim Yustic
Mwakanjuki amesema lengo la seminar hiyo nikuwafundisha waamuzi sheria mpya za
mchezo huo ambazo zinaanza kutimu kuanzia mwaka huu.
Amesema kozi hiyo ya
waamuzi inatarajiwa kuchukua wiki moja ambapo inatarajiwa kuanza July 10 ambapo
yataendeshwa katika ukumbi wa Polis skwash.
Ameongeza kuwa mafunzo
hayo yanatarjiwa kuendeshwa na mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya chama cha mchezo
huo Ali Muhamed ambapo jumla ya waamuzi 15.
Ameeleza kuwa baada
yakumalizika kwa kozi hiyo chama chao kitaendesha mafunzo kwa kama hayo kwa
viongozi wa vilabu.
Amewataka wadau na
wapenzi wa mchezo huo kuunga mkono jitihda zao ilikufanikisha malengo ambayo
chama chao yamejiekea.
No comments:
Post a Comment