Bank ya NMB imewapatia
vifaa vya kimichezo timu ya Jamhuri inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa
ajili ya michezo iliyosalia ya ligi kuu.
![]() |
Manager wa NMB Ahmed Nassor alieva koti jeusi akimkabidhi jezi manager wa Jamhuri Abdallah Muhamed Elisha |
Akizungumza na mtandao huu
manager wa timu ya Jamhuri Abdallah Muhamed Elisha amesema wamefikia makubali
na bank hiyo na kwa sasa timu yake itavaa jezi yenye nembo ya bank hiyo ya NMB.
Kuhusu makubaliano ambayo
wamekubaliana na bank hiyo amesema kwa sasa ni mapema kuyaweka yote hadharani
lakini bank hiyo itagharamia usafiri wa timu hiyo kwenda nakurudi katika
michezo yake yote ya ligi kuu soka ya Zanzibar.
Sambamba na hayo pia bank
hiyo imekabidhi viatu kwa ajili ya wachezaji wa timu hiyo sambamba fulana zakuchezea katika michezo yake ya ligi
kuu soka ya Zanzibar.
Amewataka wadau na
washabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuinga mkono timu hiyo iwapo uwanjani
ilikufikia malengo waliyojiekea yakutwa ubingwa wa ligi kuu soka ya Zanzibar
kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment