Mshambuliji hatari wa timu
ya Jamhuri Khamis Abdallah Mbulu ataukosa mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kati
ya timu ya Jamhuri na timu ya Zimamoto mtanange ambao utavurumishwa katika
dimba la Amani mjini Unguja July,10 mwaka huu.
![]() |
Kikosi cha Jamhuri kinachotarajiwa kuwasili kisiwani Unguja kesho tayari kwa michezo yake miwili ya ligi kuu soka ya Zanzibar. |
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na manager wa timu hiyo Abdallah Muhamed Elisha yenye maskani yake
Wete kisiwani Pemba nyota huyo amepata majeraha katika mazoezi ya timu hiyo hapo
jana na kwa mujibu wa report ya daktari nyota huyo anatarajiwa kukaa nje ya
uwanja kwa takribani wiki moja.
Ameongeza kuwa kikosi
hicho cha vinara wa ligi kuu soka ya Zanzibar
kinatarajiwa kuondoka kisiwani Pemba asubuhi ya kesho ,July 6 ,kuja
Unguja kwa meli ya Azam Sea Link na wanatarajiwa kusafiri na msafara wa
wachezaji 25 na viongozi watano ambapo watafikia katika hostel za chuo cha
mafunzo.
Jamhuri inaongoza ligi kuu
soka ya Zanzibar wakiwa na alama 9 baada yakushinda katika michezo yake mitatu
waliyocheza ,wanakuja kisiwani Unguja kucheza michezo miwili ambapo July,10
watacheza na mabingwa watetezi timu ya Zimamoto huku July 13 wakikipiga na
Taifa ya Jang’ombe kabla yakurudi kisiwani Pemba .
No comments:
Post a Comment