Thursday, 8 June 2017

Kamati beach soccer uso kwa uso na waziri.



Kamati inayosimamia soka la ufukweni visiwani Zanzibar wanatarajiwa kukutana na waziri wa habari utamaduni utalii na michezo lengo ikiwa ni kujadili masuala kadhaa yanayohusu soka hilo la ufukweni.
 
Timu ya taifa ya Zanzibar ya soka la ufukweni.
Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa kamati hiyo ya soka la ufukweni Ali Sharif Adolf amesema ameona haja yakukutana na waziri anaehusiana na michezo,ZFA taifa,baraza la michezo sambamba na wadau wengine wa michezo ilikuimarisha mchezo huo wa ufukweni.

Ameongeza kuwa katika miaka mitatu tokea kuazishwa kwa kamati hiyo ya soka la ufukweni mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo kukua kwa mchezo huo sambamba na kuchezwa kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya Zanzibar ya na ile ya Uganda.


Amewataka wadau mbali mbali wa soka nchini kujitokeza kwa wingi katika kuimarisha mchezo huo wa soka la vijana nakuitangaza Zanzibar kimataifa.

No comments:

Post a Comment