Kikosi cha combine ya
wilaya ya mjini kinaendelea na maandalizi yake kujiandaa na mashindano ya
Rolling Stone yanayotarajiwa kufanyika July 9 hadi 19,Mbulu Manyara.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na katibu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya mjini Unguja Yahya
Juma kikosi hicho kinaendelea na maandalizi na kinatarajiwa kucheza michezo
miwili ya mwisho ya kirafiki kabla yakuondoka July 6 kuelekea katika mashindano
hayo.
Amesema michezo hiyo
ya kirafiki ni ule utakaovurumishwa kesho July 3 mnamo majira ya saa kumi
alasiri ambapo combine hiyo itamenyana na timu ya Dulla boys sambamba na ule wa
July 5 ambapo timu hiyo itajipima nguvu na timu ya Taifa ya Jang’ombe.
Amesema kikosi cha
wachezaji 20,na viongozi 5 wanatarajiwa kuondoka July ,6 kuelekea katika
mashindano hayo ambapo mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya mjini
Hassan Haji Hamza akitarajiwa kuongoza kikosi hicho kuelekea katika mashindano
hayo.
Wadau wa soka please tuichangie timu yetu hii ikatuwakilishe kwa vizuri na kuitangaza Zanzibar nje ya mipaka yake
ReplyDelete