Saturday, 1 July 2017

Uchaguzi BAZA mjini ,wapingwa kalenda.


Kamati ya uchaguzi ya chama cha mpira wa kikapu visiwani imeghairisha uchaguzi uliokuwa ufanyike asubuhi ya jana ambao ungepelekea kupatikana kwa viongozi watakaongoza mchezo wa kikapu katika wa wilaya ya mjini kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
 
KATIBU WA KAMATI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU ZANZIBAR KIBABU HAJI HASSAN.
Akitolea ufafanuzi juu yakuhairishwa kwa uchaguzi huo katibu wa kamati ya uchaguzi Kibabu Hajji Hassan amesema wameamua kuhairisha uchaguzi huo kutokana nakutokukamilika kwa idadi inayotakiwa ya wajumbe ambao wanasifa zakupiga kura.

Amesema kuwa kwa mujibu wa mrajisi wa vyama vya michezo vilabu ambavyo vimefanyiwa usajili ni 20 huku waliohudhuria katika uchaguzi huo vikiwa 6 tu jambo ambalo kwa mujibu wa katiba itakuwa havijafikia matakwa ya katiba katika kuendesha zoezi hilo.

Ameongeza kuwa katika vilabu sita vilivyohudhuria katika zoezi hilo ,vilabu vitatu havikukamilisha taratibu za kisheria jambo ambalo lingepelekea kupatika kwa viongozi kinyume na sheria nakulazimika kusitisha zoezi hilo la uchaguzi.

Kwa upande mwengine kibabu amesema wao hutakiwa kutoa taarifa za uchaguzi kwa wilaya mara baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa kamati tendaji iliyomaliza muda wake nakutokuhudhuriwa na wajumbe stahiki katika zoezi hilo wao kama kamati hawahusiki na sakata hilo.


Kwa upande wake katibu wa timu ya KVZ Mtumwa Abdallah Silima amesema kuhairishwa kwa uchaguzi huo  imewaathiri kidogo na suala hilo linatokana na  ucheleweshaji wa ufikishwaji taarifa kwa wakati.

No comments:

Post a Comment