Idadi ya makocha wenye lessen A imeongezeka visiwani
Zanzibar baada ya makocha saba kutoka
Zanzibar kuwa miongoni mwa makocha 19
waliohitimu kozi ya Daraja ‘A’ ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) iliyofanyika
Makao Makuu ya Shirikisho la Kabumbu Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala
mjini Dar es Salaam.
![]() |
Kocha Abdul Mutik Haji wa timu ya Jamhuri ni miongoni mwa makocha waliohitimu kozi ya Lessen A ya ukocha. |
Makocha hao walimaliza gwe ya pili ya siku 19, katika kozi hiyo ambayo mbali ya kuwa na wakufunzi wengine, wakufunzi wakuu wa CAF walikuwa ni Athumani Lubowa na Sunday Kayuni.
Kayuni ambaye ni Mkurugenzi wa zamani wa TFF katika kozi hii amehudumu kama mkufunzi mkuu wa CAF na aliyekuja kuwasimamia (Accessor) ni Mkurugenzi wa sasa wa Shirikisho la Soka Uganda, Athumani Lubowa.
![]() |
Malale Hamsini Keya. |
Makocha hao (7)kutoka Zanzibar
waliohitimu katika kozi hiyo ya ukocha kwa ngazi ya lessen A ni Abdul mutik Haji “Kiduu” (Jamhuri), Hababuu
Ali Omar (JMK Youth Park), Abdallah Mohammed Juma “Bares” (Prisons), Malale Hamsini
Keya (Ruvu Shooting), Ali Vuai Shein (Kijichi), Salum Juma Makame (Tanga)
pamoja na kocha Salum Ali Haji (Chwaka Stars).
Makocha wengine waliohitimu katika kozi hiyo ni pamoja na Kidao Wilfred Mzigama, Wane Nelson Mkisi, Meck Maxime Kianga, Emmanuel Raymond Massawe, Mohammed Alawdin Tajdin, Fikiri Elias Mahiza, Juma Ramadhani Mgunda na Dismas Gordon Haonga, Abdul Hassan Banyai, Maka Andrew Mwalwisi, Dennis Mrisho Kitambi na Sebastian Leonard Nkoma.
No comments:
Post a Comment