Saturday, 24 June 2017

ZFA IBADILIKE ILIKUIMARISHA SOKA LETU,KOCHA BUSHIR.

Kocha mkuu wa timu ya Mwadui ya Shinyanga Ali Bushir Mahmoud amewataka viongozi wa chama cha mpira wa miguu visiwani kubadilika kiutendaji ilikuimarisha soka katika visiwa vya Zanzibar.
 
Kocha Ali Bushir Mahmoud.
Bushir ametoa ushauri huo wakati alipokuwa akizungumza na zenjsport on line nakusema kuwa baada ya Zanzibar kupata uanachama wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF)  lazima viongozi wa chama cha soka kubadilika kiutendaji nakuacha kufanya kazi kimazoea ilikukuza soka la Zanzibar.

“Lazima tujieke sawa katika uongozi,tuache ubabaisha katika kuongoza soka hapa ndani lazima tujirekebishe tufanye soka la nyumbani liwe la ushindani na tuwe na nizamu sambamba na kuwa na watu wa mpira kweli ambao watafata kanuni na sheria zinazoongoza soka”Alisema Bushir.
 
Makamo wa rais wa ZFA Ali Muhammed.
Amesema kuwa umefika wakati sasa kwa Zanzibar kutengeneza katiba ambayo itakuwa imara na yenye kuangalia masilahi ya soka la Zanzibar nakuwataka viongozi wa vilabu kuwa na viongozi wanaongoza vilabu vyao wenye uweledi wakuendesha shughuli za mchezo wa soka ilikuendesha timu zao katika misingi iliyoimara.


Akizungumzia soka la vijana kocha huyo amewataka viongozi wa ZFA kuandaa mfumo nzuri ambao utasaidia kukuza soka la Zanzibar nakupelekea kuwa na timu za taifa imara katika miaka mitano ijayo.

No comments:

Post a Comment