Mlinzi mpya wa timu ya
Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja" amesema mara baada yakufanikiwa
kusaini mkataba wa miaka miwili na timu ya Yanga ya Dar es salam kwa sasa
anajipanga kuona anapata namba ya uhakika katika kikosi hicho chenye maskani
yake katika mtaa wa Jangwani.
Ninja ameyasema hayo
wakati alipokuwa akizungumza na zenjsport -on line nakusema anajua atakabiliana
na changamoto katika kikosi hicho lakini atahakikisha anajituma ili awe chaguo
namba moja la kocha wa kikosi chake hicho kipya.
Amesema moja ya ndoto
zake nikucheza katika timu kubwa lakini kufika kwake yanga ni miongoni mwa njia
zakufikia kule alikojipangia.
“Yanga ni kama njia kwangu yakusonga mbele
zaidi lengo langu nikucheza soka nje ya Tanzania naamini kujituma kwangu ndiko
kutakakosaidia kufikia malengo yangu “Alisema Ninja.
Aidha nyota huyo amewaomba
mashabiki wa soka visiwani na wapenzi wake kumuombea dua ilikufanikisha malengo
yake aliyojiekea nakusema kuwa atahakikisha anapambana ipasavyo ilikufikia
malengo yake.
Ninja ndie mchezaji wa
kwanza msimu huu wa mwaka 2017-2018 kusajiliwa Yanga akitokea Taifa ya
Jang’ombe ya Zanzibar ambapo amefunga mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu
hiyo.
No comments:
Post a Comment