Saturday, 1 July 2017

Akina Park Ji Sung walazimishwa sare na Taifa.

Timu ya taifa ya Jang’ombe inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar imeshindwa kuwatambia Halelujah FC inayoshiriki ligi daraja la Pili nchini Korea ya kusini katika mchezo wa maalum wa kirafiki mchezo ulivurumishwa katika dimba la Amani mjini Unguja.
Wachezaji wa Halelujah FC .

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani huku safu ya ulinzi ya Halelujah FC ikionekana imara hadi dakika tisini za muamuzi Rashid Farahan Webb zinakamilika hakuna timu iliyoona lango la mweziwe.
Nyota wa Halelujah FC 

Halelujah FC ipo Zanzibar kwa ziara maalumu ambapo itacheza tena mchezo wa kirafiki July,4 na timu ya Polis mchezo ambao pia utachezwa katika kiwanja cha Amani mjini Unguja mnamo majira ya saa kumi alasiri kabla yakusafiri kuelekea Tanzania bara kupiga mchezo wa kirafiki na timu ya Yanga ya jiji Dar es Salam.


No comments:

Post a Comment