Sunday, 2 July 2017

MKURUGENZI WA UFUNDI MIEMBENI CITY AACHIA NGAZI

Mkurugenzi wa ufundi wa timu ya Miembeni City ambayo itashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa mara ya kwanza katika msimu ujao wa ligi Ali Mohammed ameachia nafasi hiyo aliyokuwa akiishikilia kwa takribani miaka miwili sasa.

Akizungumza na mtandao huu juu ya sababu ambayo imemfanya kuachia nafasi hiyo aliekuwa mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo amesema ameamua kuacha nafasi hiyo ilikulinda matakwa ya katiba ya timu yao hiyo.

“Nimeachia nafasi hii ilikuendana na matakwa ya katiba ya timu yetu ,unajua katiba ya timu yetu inasema nafasi ya mkurugenzi wa ufundi ni nafasi yakuajiriwa hivyo nimeachia ili kutoa fursa kwa wenye sifa pale itakapotangazwa nafasi sambamba na kukidhi mahitaji ya katiba yetu”aliseama.

Sambamba na hayo amesema kwa kipindi kirefu alikuwa akivaa kofia mbili katika timu jambo ambalo ni kinyume na katiba ya timu hiyo hivyo kuachia nafasi hiyo kutoa fursa yakubakia na nafasi yake yakuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo.

Amewaomba walimu wenye sifa kujitokeza kuomba nafasi hiyo pale itakapotangazwa ilikuendeleza maendeleo ya timu hiyo.

No comments:

Post a Comment