Mabingwa watetezi wa Ligi kuu soka ya Tanzani
Bara timu ya Yanga Sports Club wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya
Mabingwa wa zamani wa Zanzibar timu ya Mlandege Sports Club mchezo ambao
utasukumwa Jumapili Agost 13, 2017 saa 2:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan.
Yanga ambao wanatarajia kuweka kambi Kisiwani
Pemba watalazimika kukaa siku moja Kisiwani Unguja kwaajili ya mchezo huo kisha
kuendelea na safari ya kwenda Pemba kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani
dhidi ya mpinzani wao wa Jadi Simba.
Akizungumza na Mtandao huu Katibu wa Soka
Wilaya ya Mjini Yahya Juma Ali ambae yeye ndie mratibu wa mchezo huo amesema
Yanga watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege na matayarisho ya mchezo
huo yanaendelea vizuri kwani tayari washawatafutia Hoteli ya kuiweka Yanga siku
moja itakapokaa Unguja.
“Yanga watacheza na Mlandege Jumapili usiku
katika uwanja wa Amaan, matayarisho yapo vizuri sana kwani mpaka Hoteli
tushawaekea Yanga kwa siku moja watakayokaa Unguja kisha wataenda Pemba
kwaajili ya kambi”. Alisema Yahya.
Simba na Yanga zitakutana katika mechi ya Ngao
ya Jamii Agosti 23, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salam mchezo
ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment