Saturday, 12 August 2017

Alfred Kapinga aridhishwa na kambi ya wanamichezo Zanzibar.

Mkuu wa operesheni na mafunzo pamoja na michezo ndani ya jeshi la wananchi wa Tanzania Brigidia General Alfred Kapinga  amewataka wachezaji wa timu ya majeshi ya Tanzania kuongeza bidii na nidhamu katika mazoezi ilikufanya vyema katika mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki na kati.


Hayo ameyaeleza wakati alipokuwa akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo katika kambi ya wanamichezo wa majeshi iliyopo Zanzibar.

Amewataka wanamichezo hao kujituma kwa vile michezo ni sehemu ya kazi zao huku akielezea imani yake yakufanya vyema katika michezo hiyo.

Amesema wameamua kuzileta timu hizo za majeshi kueka kambi visiwani Zanzibar kutokana na mazingira yalivyo sambamba na ukarimu uliopo kwa wazanzibar.

Nao makocha wa timu mbali mbali za majeshi wamesema wanaenda katika mashindano hayo ya majeshi kwa nchi za afrika mashariki na kati wamesema wanaenda katika mashindano hayo kupambana ilikutwaa ubingwa.


Mashindano ya michezo ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati mwaka huu yatafanyika Bujumbura Mjini Burundi kuanzia  Agost 20, 2017 ambapo timu za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litashiriki kwa michezo mitano ikiwemo mpira wa Miguu, mpira wa Kikapu, mpira wa Wavu, mpira wa Pete na Riadha.

No comments:

Post a Comment