Sunday, 13 August 2017

Yanga waitwanga Mlandege huku Ajib akianza kupasia nyavu.

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Ibrahim Hajib leo amefunga bao lake la kwanza katika timu hiyo ikishinda 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege Uwanja wa Amaan, Zanzibar

Pamoja na kufunga dakika ya 50 akimalizia krosi ya Mzimbabwe Donald Ngoma, Hajib pia leo ametoa pasi ya bao la pili lililofungwa na winga machachari, Emmanuel Mrtin dakika ya 73.

Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika timu hizo zikiwa hazijafungana, kocha Mzambia, George Lwandamina leo alibadilisha wachezaji wote kipindi cha pili, kasoro kipa Ramadhan Awam Kabwili.

Na ni mabadiliko aliyoyafanya ndiyo yaliipa ushindi timu yake katika mchezo huo wa kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Simba Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa timu ya yanga  George Lwandamina amesema ameutumia mchezo kuangalia uimara wa wachezaji wake.

Nae kocha wa timu ya Malandege Jaala Salum amesema mchezo huo wameutumia kukitengeneza kikosi chao kuelekea msimu ujao wa ligi.

Yanga iko Zanzibar ikiendelea na maandalizi ya kujiwinda na pambano lao la ngao ya jamii dhidi ya Simba litakalopigwa agost 23 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo asubuhi ya leo kikosi hicho kitaelekea kisiwani Pemba kwa kambi kabla ya kurejea jijini Dar es salaam siku mbili kabla ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa hali juu.
.

No comments:

Post a Comment