Saturday, 10 June 2017

Rais wa Miembeni City aichangia Combine ya Rolling.



Katika kuhakikisha anatoa michango yake katika kuendeleza maendeleo ya soka la Zanzibar Rais wa timu ya Miembeni City Seif Kombo (Seif Bosi)asubuhi ya leo ametoa mchango wake kwa timu ya Combine ya wilaya ya mjini inayotarajiwa kuelekea Mbuli mkoani Manyara baada yakumalizka kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya mjini Unguja Hassan Haji alieva kapelo  akipokea fedha kwa rais wa timu ya Miembeni City Seif Kombo.

 
Rais wa Miembeni City alikabidhi mchango wake huo kwa mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya mjini Unguja Hassan Haji(Chura) mara baada yakumalizika kwa mazoezi ya vijana hao yanayoendelea kila siku katika kiwanja hicho.

Akipokea mchango huo mwenyekiti huyo amemshukuru rais huyo nakuwataka wadau mbali mbali wa soka kuunga mkono kikosi hicho ilikufanikisha safari yakuenda kulitetea taji hilo walilotwaa katika mashindano yaliyopita.
Kocha wa timu ya combine ya wilaya ya mjini Muhamed Seif King akizungumza na wachezaji wa timu hiyo baada ya mazoezi.


Ameongeza kuwa bado timu hiyo inahitaji michango ya hali na mali ilikufanikisha safari ya mabingwa hao watetezi wa mashindano hayo.

Kikosi cha combine ya wilaya ya Mjini kiundwa na walinda milango Alley Ally(Miembeni City)Makkame Mikidadi(Huru)Peter Dotto(Schake 04) walinzi Muharamami Khamis(Blacksaloir)Abdulkhamid Salum(KVZ)Ali Hassan(Uhamiaji)Hassan Haji(Kipanga)Ismail Mchana(Mwembebeni)Abubakary Ame(Miembeni City)Ali Juma(Taifa ya Jang’ombe)Shaaban Pandu(Villa United)


Wengine Yakoub Amour(Jang’ombe Boys),Ibrahim Ali(Villa Central)Suleiman Ali(Jang’ombe boys)Mussa Shaaban Vicent(Zimamoto)Muhamed Haji(Jang’ombe boys)Muhamed Mussa(Mapembeani)Talib Hamad(Kipanga)Seif Said (KVZ)Fahmi Salum(Mlandege)Abdurahama Juma(KMKM)Muhamed Jailan(Chriss fc)Juma Ali (Villa United)Suleiman Ali(Uhamiaji)Ibrahim Abdallah(Miembeni City)Muhamed Ridhaa(Villa United)

No comments:

Post a Comment