Mabingwa
wa mashindano ya karume cup kwa upande
wa mpira wa kikapu timu ya polisi ya zanzibar imepania kufanya vizuri katika
michezo ya ligi kuu ya Zanzibar kwa mchezo huo.
Akizungumza
na mtandao huu msemaji wa timu hiyo Hamid Fadhil amesema baada yakukamilika kwa
mashindano ya ya Karume cup na timu yao kutwaa ubingwa kwa sasa wanajipanga kukisuka kikosi chao
hicho.
Amesema
kuwa tayari kamati ya usajili ya timu hiyo imeshakutana na viongozi wao
ilikupanga masuala kadhaa yanayohusu usajili huku wakitarajia kuwajumusiha
nyota kadhaa wapya katika kikosi chao hicho.
Kuhusu
mashindano ya karume cup msemaji huyo amesema mashindano hayo yanahamasa kubwa
na kutwaa ubingwa katika michezo hiyo kunazidi kuamsha hamasa kwao.
Amewataka
wadau na wapenzi wa timu hiyo kuendelea kuwaunga mkono ilikuweza kufanya vyema
katika mashindano hayo ya ligi kuu ya mchezo huo kwa upande wa kanda ya Unguja.
No comments:
Post a Comment