Saturday, 10 June 2017

HIPZ kukusanya pesa kwa ajili ya huduma za afya Zanzibar kupitia mbio za Baiskeli

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar. 
Mradi wa Kuimarisha huduma za Afya Zanzibar (HIPZ) unatarajia kukusanya zaidi ya dola za Marekani 25,000 kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika Hospitali ya Makunduchi na Kivunge ambazo wanazisaidia.
Washiriki wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) wakikata maeneo ya viwanja vya Maisra kuendelea na safari yao itakayochukua siku sita.
Picha na Makame Mshenga.

Fedha hizo zitapatikana kufuatia kuandaa resi za baiskeli za kilomita 300 (Bike Ride 2017) katika mikoa mitatu ya Unguja yatakayo dumu kwa muda wa siku sita kuanzia leo.
Akizungumza na waandishi wa habari Hoteli ya Tembo, Mratibu wa resi hizo Dkt. Jon Rees kutoka Uingereza  amesema jumla ya wapanda baiskeli 25 kutoka Ulaya na Zanzibar wanashiriki.
Mratibu wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) Dkt. Jon Rees akizungumza na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya mbio hizo Zanzibar ikiwa ni mara yake ya tatu.
Picha na Makame Mshenga

Amesema fedha hizo zitachangwa na makampuni ya ndani na nje ya nchi  na zitatumika kuimarisha huduma za afya hasa  afya ya mama na mtoto katika Hospitali za Kivunge na Makunduchi.
Amesema Resi hizo ambazo ni mara ya tatu kufanya  Zanzibar zilianzia Mji Mkongwe kuzunguka maeneo mbali mbali ya Mkoa Mjini Magharibi zitapitia Nungwi, Makunduchi, Kizimkazi na zitrejea Mji Mkongwe.
Picha ya pamoja ya washiriki wa Bike Ride 2017 wakifurahia mbio hizo kabla ya kuanza rasmi.
Picha na Makame Mshenga

Dkt. Ress amewataka wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwatia hamasa wapanda baiskeli hao hasa katika sehemu watakazopita.
Akizindua resi hizo, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla Mohd amesema Mradi wa HIPZ  umeleta mafanikio makubwa katika ubunifu wake wa kutafuta fedha kwa ajili ya  huduma za afya kwa kuanzisha mbio hizo.

No comments:

Post a Comment