Jumla ya
vijana 30 wamefanikiwa kupata nafasi yakujiunga na kituo cha kukuza vipaji vya
michezo Zanzibar(ZFDC) katika zoezi lakutafuta vijana hao lililofanyika asubuhi
ya leo katika uwanja wa Amani mjini Unguja.
Zoezi hilo
lakusaka vipaji lilisimamiwa na makocha kadhaa wa mpira visiwani na vijana
waliobahatika kupata nafasi yakujiunga katika kituo hicho watapatiwa hudu zote
za msingi ambazo zinahitajika kwa wanamichezo.
Akizungumza na
mtandao huu manager wa kituo hicho cha kukuza vijana Omar Bakar amesema vijana
hao 30 ambao wamewapata leo watajumuika na wengine watakaopatikana katika zoezi
kama lililofanyika asubuhi ya leo wiki ijao.
Ameongeza kuwa lengo la kituo chake hicho
nikukusanya jumla ya vijana 50 wenye miaka chini ya umri 20 lengo nikuwajengea
misingi imara yakucheza mchezo wa soka.
No comments:
Post a Comment