Wakiwa wametoka kutoka katika mashindano ya Sport Pesa Super Cup timu ya Jang’ombe Boys wanatarajiwa kuanza mazoezi yao yakujiandaa na michezo ya hatua ya nane bora yanayotarajiwa kuanza kuanzia July ,9 mwaka huu.
![]() |
Abdi Kassim Babi wa Jng'ombe boys akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Gor Mahia. |
Aidha ameongeza kuwa kikosi chao hicho kinatarajiwa kuondoka visiwani Zanzibar Juni ,27 kuelekea Tanzania bara kwa ajili ya kambi ya wiki moja ambapo wakitoka katika kambi yao hiyo wataelekea moja kwa moja kisiwani Pemba.
![]() |
Kikosi cha Jnag'ombe boys. |
Ameongeza kuwa katika kambi yao hiyo ya wiki moja Tanzania bara wanatarajia kucheza michezo mitatu ya kirafiki ambapo kama taratibu za kiuongozi zitaenda kama wanavyopanga watacheza na timu ya Simba,Yanga na Singida United.
“Unajua tunahitaji kufanya vyema katika michezo yetu ya hatua ya nane bora ilitujikatie tiketi yakushiriki katika mashindano ya kimataifa na katika kujiandaa tutaeka kambi ya wiki moja Tanzania bara kuona timu inapata maandalizi mazuri na katika kambi hiyo tunatarajia kucheza na Simba,Yanga na Singida United” alisema rais huyo.
Akizungumzia mashindano ya Sport Pesa Super Cup ambayo timu hiyo imeshiriki nakutolewa mapema rais huyo amesema kubadilishwa kwa ratiba nakutoruhusiwa kuwatumia baadhi ya nyota wao ambao walisafiri nao ndio sababu kuu iliyopelekeakea kupoteza katika mchezo wao na Gor Mahia.
Akizungumzia suala lakutomtumia mlinzi wao wa kati Ali Humud Badru rais huyo amesema nikutokana na nyota huyo kuhitajika kufanya majaribio katika kilabu ya Simba na katika kipindi hicho cha mashindano nyota huyo alikuwa katika timu hiyo.
No comments:
Post a Comment