Sunday, 11 June 2017

Kilimani City kutafuta viongozi wapya, August



Timu ya Kilimani City inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar ipo katika mipango yakufanikisha uchaguzi mkuu kwa ajili yakupata viongozi wapya watakaoongoza timu hiyo kwa mujibu wa katiba ya timu hiyo.
 
Rais wa timu Kilimani City Khamis Shaali akiwa na mshauri mwelekezi wa kampuni ya Alfa Zanzibar Suleiman Shaaban Suleiman.

Hayo yamebainishwa na rais wa timu hiyo Khamis Shaali wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema kuwa kwa sasa timu yao inaliangalia suala hilo ili kuendeleza timu yao hiyo.

Amefafanua kuwa uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika August mwaka huu ambapo nafasi ambazo zitagombaniwa katika uchaguzi huo ni pamoja na rais ,makamo wa rais,katibu,msaidizi katibu,mshika fedha pamoja wajumbe wa kamati tendaji ya timu hiyo.


Akizungumzia suala la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi rais huyo amesema kwa sasa hawajalijadili suala hilo kwa vile hawajajua timu yao itacheza ligi gani hivyo watafanya usajili pale endapo hawajajijua watacheza ligi gani.

“Unajua hatuwezi kusajili kwa sasa kwa sababu hatujui tusajili mchezaji wa aina gani kwa vile bado hatujajua tutacheza ligi gani kwa sababu bado ZFA ipo kimpya kihabari tunasikia tu kutoka kwa watu wa pembeni”Alisema rais huyo.

Aidha amewaomba washabiki na wapenzi wa timu hiyo kuiunga mkono timu yao hiyo kwa hali na mali ilikufanya vyema katika msimu ujao wa ligi.

1 comment: