Saturday, 10 June 2017

ZFDC kusaka vipaji vya soka.

Kituo cha kukuza vipaji vya michezo Zanzibar(ZFDC) wanaendelea na mipango yao yakuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana wakizanzibar ambapo asubuhi ya kesho wanatarajiwa kuendesha mchujo kwa ajili ya nyota wapya watakaojumuika katika kituo hicho.

Akizungumza nasi mkurugenzi wa kituo hicho Omar Bakar amesema wanatarajiwa kukusanya vijana wa chini ya miaka 12 mpaka 20 ambapo katika mchujo wao wa hapo kesho wamepanga kukusanya vijana ambao watakuwa na uwezo wa hali ya juu yakusakata soka.

Ameongeza kuwa katika kituo chao hicho ambacho kinatarajiwa kukusanya jumla ya nyota 50 ambao watakuwa na umri wa chini ya miaka 20 kina lengo lakuimarisha soka la vijana katika kisiwa cha Unguja.



Aidha amewaomba wazazi kujitokeza kuwapeleka watoto wao kujaribu bahati yao ilikujumuika na nyota waliopo katika kituo hicho.

No comments:

Post a Comment