Monday, 5 June 2017

Wilaya ya mjini yazidi kujino kwa ajili ya Rolling Stone.

Combine ya wilaya ya mjini itakayoshiriki katika mashindano ya Rolling Stone inaendelea kujinoa kujiandaa na mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika kuanzia  June 29, Jiji Arusha.

Kocha wa combine ya wilaya ya mjini Muhamed Seif King akizungumza na wachezaji wa timu hiyo baada ya mazoezi ya asubuhi.

Akizungumza na mtandao huu kocha msaidizi wa timu hiyo Ramadhani Madundo amesema kikosi chao kipo katika maandalizi mazuri huku wakizidi kujipanga kufanya vyema katika mashindano hayo.

“Kikosi kinaendelea na mazoezi chini ya mimi na kocha mkuu Muhamed Seif King vijana wanajituma vilivyo katika mazoezi na hali ya wachezaji ipo vizuri kinachohitajika nikuungwa mkono ilikufanya kama tulichofanya mashindano yaliyopita”alisema Madundo.

Wachezaji wa combine ya wilaya ya mjini wakimsikiliza mwalimu wa timu hiyo hayupo pichani.


Akizungumzia kikosi hicho kocha huyo amesema kikosi kipo vizuri na kimesheni wanandinga kadhaa wenye uwezo wa hali juu jambo ambalo linawapa imani yakufanya vyema katika mashindano hayo.

Kikosi cha Mjini Unguja (Mabingwa watetezi) mpaka sasa kina jumla ya nyota 26 wakiwemo walinda mlango Aley Ali Suleiman “Manula” (Miembeni city), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na Makame Mkadar Koyo (Huru).

Kikosi cha Mjini Unguja (Mabingwa watetezi) mpaka sasa kina jumla ya nyota 26 wakiwemo walinda mlango Aley Ali Suleiman “Manula” (Miembeni city), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na Makame Mkadar Koyo (Huru).

Nyota wa combine ya wilaya ya mjini wakiwa na mwalimu wao.



Wengine ni Mohd Jailan (Chrisc), Makame Masoud (Schalke 04), Mohd Mussa (Mapembeani), Abrahman Juma (KMKM), Mohd Haji (Jang’ombe Boys), Abdul-hamid Juma (ZAFSA), Ibrahim Chafu (Villa FC) ,Ibrahim Abdallah(Miembeni Cit),Asaad Juma (Kilimani City)na Juma Ali Yussuf “James” (Villa United).

No comments:

Post a Comment