Bodi ya
wakurugenzi ya timu ya Miembeni City imekutana jioni ya jana kupitia ripoti ya
mwalimu sambamba na kujadili masuala kadhaa yahusuyo timu ikiwa na suala la
usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
![]() |
Wachezaji wa Miembeni City wakiingia uwanja. |
Katika kikao
hicho bodi hiyo imeipitia riport ya mwalimu aliyowasilisha nakuungana na
mapendekezo ya mwalimu yakuacha nyota sita nakuongeza wengine kumi kulingana na
nafasi alizopendekeza mwalimu.
Akizungumza na
mtandao huu mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Ali Muhamad amesema wajumbe wa bodi ya wakurungezi wa timu
imerizia mapendekezo ya mwalimu ikiwemo kuacha nyota wao sita huku wakiongeza
wengine kumi wapya.
![]() |
Nyota wa Miembeni City. |
“Ni kweli
bodi imekubaliana na ripoti ya mwalimu na kwa sasa tupo katika kuyafanyia kazi
mapendekezo ya mwalimu ikiwemo kuacha nyota hao sita huku nyota wawili
tukiwaeka sokoni kutokana na mikataba yao kuwa ya muda mrefu katika timu yao
hiyo”alisema mkurugenzi huyo waufundi.
Akiwataja nyota
ambao watawaacha katika kikosi chao ni pamoja na Khamis Hamad Muhamed,Khamis
Muhamed Ali,Yussuf Mussa kheri,Ali Muhamed Juma,Yussuf Dotto Shaaban na Yussuf
Kassim Yussuf.
![]() |
Nahodha wa timu ya Miembeni City Habibu Ali |
Ameongeza kuwa
wachezaji Adam Khamis Mohamed na Farid Uled Wadi wamewaeka sokoni kwa timu
ambayo itawahidi kufanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo.
Amefafanua kuwa
wapo katika mazungumzo na baadhi ya nyota kuwajumuisha katika kikosi chao na
endapo watafikia makubaliano nakufungana nao mkataba watawaeka wazi nyota.
![]() |
Mkurugenzi wa ufundi wa Miembeni City akiwa na mlinzi wa timu hiyo Abubakary Ame. |
Kuhusu kutakiwa
kwa baadhi ya nyota wake na timu nyengine zinazocheza ligi kuu soka ya Zanzibar
mkurungezi huyo amesema uongozi wa timu haujapata ofa mpaka sasa kutoka timu
yoyote na endapo itatokea watakaa nao mezani kuona uwezekano wakufanya
mazungumzo na timu hiyo.
No comments:
Post a Comment